Judges 11:1-6

1 aBasi Yefta Mgileadi alikuwa mtu shujaa. Baba yake alikuwa Gileadi, naye mama yake alikuwa kahaba. 2Mke wa Gileadi akamzalia wana wengine, nao watoto hao walipokua, wakamfukuza Yefta na kumwambia, “Wewe huwezi kupata urithi katika jamii yetu, kwa sababu wewe ni mwana wa mwanamke mwingine.” 3 bBasi Yefta akawakimbia ndugu zake akaenda kuishi katika nchi ya Tobu, mahali ambako watu waasi walijiunga naye na kumfuata.

4 cBaada ya muda Waamoni wakafanya vita na Israeli, 5viongozi wa Gileadi wakaenda kumchukua Yefta katika nchi ya Tobu. 6Wakamwambia Yefta, “Uwe jemadari wetu, ili tuweze kupigana na Waamoni.”

Copyright information for SwhKC